Tetesi za soka ulaya alhamisi ya tarehe 18.01.2018


Mkataba wa Manchester United wa kumsajili mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez utafikia pauni milioni 180 baada ya mchezaji huyo kusaini mkataba wa miaka minne na nusu. (Telegraph)

Alexis Sanchez atalipwa zaidi ya pauni 400,000 kwa wiki Manchester United. (Independent)

Liverpool wamewaambia Sevilla kuwa hawapo tayari kuwapa Daniel Sturridge, 28, kwa mkopo hadi mwisho wa msimu. (Mail)

Mshambuliaji wa West Ham anayenyatiwa na Chelsea Andy Carroll amesema hawezi kufanya mazoezi huku klabu yake ikisema vipimo vinaonesha hana majeraha yoyote. (Mirror)

Chelsea wamepanda dau rasmi kumtaka beki wa Roma Emerson Palmieri. (Calciomercato)

Manchester United wameanza mazungumzo ya kumuongezea mkataba kipa David de Gea, 27. (Telegraph)

Meneja wa West Ham David Moyes alikuwepo Stamford Bridge siku ya Jumatano kumtazama mshambuliaji anayemfuatilia Mitchy Batshuayi, 24, katika mchezo dhidi ya Norwich. (Mail)

Real Madrid wanaamini muda sasa umewadia wa kuziba pengo la ‘BBC’ kwa kuwasajili Neymar, 25, kutoka PSG, Eden Hazard, 27, kutoka Chelsea na Robert Lewandowski, 29, kutoka Bayern Munich. (Marca)

Chelsea wanapambana na Manchester City katika kutaka kumsajili Jean-Michael Seri kutoka PSG. (The Sun)

Liverpool ni miongoni mwa timu zinazomtaka James Rodriguez kwa mkataba wa kudumu kutoka Bayern Munich anapocheza kwa mkopo kutoka Real Madrid. (Don Balon)

Everton wamemuulizia beki wa kushoto wa Bayern Munich Juan Bernat. (Liverpool Echo)

Liverpool wana wasiwasi huenda wakamkosa kiungo wa Schalke Leon Goretzka, 22. (Liverpool Echo)

Beki wa Arsenal Hector Bellerin, 22, ananyatiwa na Juventus na huenda wakamtaka mwisho wa msimu. Juve wamekuwa wakimfuatilia beki huyo tangu mwaka 2014. (Tuttosport)

Juventus pia wanamfuatilia kiungo mchezeshaji wa Tottenham Christian Eriksen, 25, au vinginevyo watamtaka Mesut Ozil kuwa namba 10 wao mpya. (Corriere dello Sport)

Meneja mpya wa Stoke City Paul Lambert anakaribia kukamilisha usajili wa beki wa Augsburg Kostas Stafylidis, 24, kwa mkopo hadi mwisho wa msimu. (Sun)

West Ham wanataka kumsajili kiungo wa Inter Milan Joao Mario, 24, kwa mkopo. (Telegraph)

Mshambuliaji wa West Ham Javier Hernandez, 29, huenda akaondoka huku Besitkas ikituma ujumbe London wa kuzungumza na mchezaji huyo kutoka Mexico. (Talksport)

Besitkas pia wanamtaka mshambuliaji wa Leicester City Islam Slimani, 29. (Sky Sports)

West Brom wanataka kumsajili kwa mkopo beki wa Zamalek ya Misri Ali Gabr, 26. (Express)

Mshambuliaji kutoka Brazil Richarlson, 20, anataka kuondoka Watford mwisho wa msimu huku wawakilishi wake wakianza mazungumzo na Chelsea na Arsenal. (Watford Observer)