DE GEA NA LENGO LA GOLDEN GLOVE

DE GEA NA LENGO LA KUSHINDA USHINDI WAKE WA KWANZA WA MIKONO YA DHAHABU (GOLDEN GLOVE) 


kipa Wa Manchester United  David De Gea amekiri kuwa angependa saana Kama angeshinda tuzo ya mikonob ya dhahabu (Golden Glove) kwa mara ya kwanza.

Kipa huyo namba.1 Wa Hispania Ana kumbukumbu ya kucheza bila kufungwa Mara 13  msimu huu katika Ligi Kuu na anaongoza njia katika mbio za kuwania tuzo kwa mwaka 2017/18 , kitu ambacho kinamuwekea kumbukumbu nzuri  tangu kuwasili England mwaka 2011.

"Bila shaka, mimi napenda Sana kushinda," alisema kuiambia MUTV. "Si tu mwaka huu bali kila mwaka!

"Mimi nahisi Ni jinsi timu inavyojilinda   na kuitetea timu nzima kwa ujumla na wakati kipa anapofanikiwa kutwaa tuzo kama hii. Mimi nahisi Ni ishara kwamba timu ilijilinda vizuri msimu huu  na itakuwa Ni tuzo kwa wenzangu  wote ,na hasa wale walio katika safu ya ulinzi ambao tunashirikiana katika ulinzi."



2017/18 KUCHEZA BILA KUFUNGWA:


13 - David De Gea (united)
12 - Thibaut Courtois (Chelsea)
10 - Ederson (Manchester City)
9 - Petr Cech (Arsenal), Hugo Lloris (Tottenham), Nick Papa (Burnley)

HIVI KARIBUNI WASHINDI WA MIKONO YA DHAHABU (GOLDEN GLOVE ):


2016/17 - Thibaut Courtois (Chelsea - 16)
2015/16 - Petr Cech (Arsenal - 16)
2014/15 - Joe Hart (Manchester City - 14)
2013/14 - Wojciech Szczesny (Arsenal - 16) na Petr Cech (Chelsea - 16)
2012/13 - Joe Hart (Manchester City - 18)

De Gea, ambaye Hajawai fungwa tangu mwaka 2018 uanze , hivi sasa atakuwa na lengo la kuongeza michezo ya bila kufungwa kufunga wakati united watachuana uso kwa uso na Burnley kesho (jumamosi) ya tarehe 20 mwezi Wa kwanza jioni,


                         [Man utd]