TAHADHARI

*Picha hii haihusiani na tukio hilo*

Kuna mtindo mpya wa wizi umevamia Masherehe mbalimbali


Katika sherehe ya harusi ikiwa inaendelea majambazi uja na kuongea na MC wa harusi kuwa kuna gari namba fulani fulani nje ya ukumbi limezuia gari, hivyo MC utangaza na muhusika anapokuwa anatoka nje majambazi hao ujua hakika unakuja na funguo za gari hiyo hivyo unapofika kwenye gari wao huwa wapo na bastola na kukukamata na kukulazimisha kuendesha gari pamoja nao mpaka mbali na eneo hilo kisha          kuondoka na gari.

Ni vizuri kuwa mwangalifu juu ya hili, Zingatia mambo haya:


1. Usitoke muda huo huo unaposikia kuhitajika nje kusogeza gari.

2. Usitoke pekee yako, toka hata na watu wawili au zaidi.

3. Usielekee moja kwa kwenye gari lako, kwanza tazama kwa mbali kama kweli gari lako limezuia gari la mtu na hakikisha mtu yupo katika gari hilo na angalia kama kuna watu wengine eneo la gari lako.

*Kama hauna gari shirikisha wengine suala hili.*