spurs 2 - 0 Man united : Mambo matano yaliyo ongelewa kutokana na mchezo huu

Tottenham Hotspur walijipatia goli la kwanza la mapema kabisa kabla dadika ya kwanza kuisha kupitia Eriksen, na la pili kupitia Jones baada ya kujifunga na kupelekea Manchester united kuchezea kichapo cha magoli 2 - 0, kuna mambo matano yaliyo ongelewa kutokana na mchezo huu... 

Bonyeza hapa ili kuendelea kusoma habari hii👇👇

Habari rafiki..

OKama kuna mwezi ambao unaongoza kwa kulaumiwa na kulalamikiwa kwenye miezi 12 ya mwaka, basi ni mwezi Januari. Watu wengi huwa na malalamiko kuhusu mwezi huu, na hata wengine ambao hawana sababu zozote za kushindwa kufanya kitu, basi mwezi huu huwa sababu kwao.

Mwezi huu pia umekuwa unatumika kwa utani mwingi sana kuhusu mambo kuwa magumu na mwezi kuwa mrefu. Wapo wanaosema kwamba mwezi Januari una siku 40 badala ya siku 31. Wengine wanasema kwamba mwezi Januari ni mwezi ambao huwa unagoma kuisha. Ni utani lakini ndani yake unabeba kile ambacho watu wanapambana nacho.

Ni kweli kwamba mwezi Januari huwa ni mwezi mgumu kwa watu wengi, kutokana na mahitaji makubwa ya mwezi huo, lakini pia kutokana na mwezi unaokuwa umeutangulia mwezi Januari, yaani mwezi Disemba, ambapo watu wengi wanakuwa wamefanya matumizi makubwa sana kwenye sikukuu na mapumziko ya mwisho wa mwaka.

Sina haja ya kurudia mahitaji haya ya mwezi Januari, wala ugumu wake, bali ninachotaka kukuambia leo ni kwamba, Januari imeisha. Japokuwa wengi wanaweza kushangilia kwamba Januari imeisha, lakini kuna Ujanuari ambao upo ndani ya wengi, na utaendelea kuwasumbua, na sasa watatumia jina na sababu nyingine badala ya kutumia Januari, kwa sababu imeshapita.

Leo ni siku ya mwisho kabisa ya mwezi Januari je unaamini kwamba kama Januari ilikuwa ngumu kwako basi leo ndiyo mwisho wa ugumu huo? Kwamba ukiamka kesho tarehe moja Februari basi kila kitu kitakuwa shwari? Kwamba kama ulikuwa huna fedha basi zitajaa kwenye mifuko yako?

Kama ndivyo unavyofikiria basi sina budi kukuambia kwamba unajidanganya. Na hilo siyo jipya, kwa sababu umekuwa na Januari nyingi kwenye maisha yako, na kinachofuata ni yale yale kwa jina tofauti.

Ninachokuambua rafiki yangu ni hichi, Januari imeisha lakini kuna ujanuari ambao upo ndani yako, na huu utaendelea kukusumbua kwa njia tofauti tofauti mpaka pale utakapokutana na Januari nyingine na uwe na sababu. Ninamaanisha kwamba, kama maisha yako yalikuwa magumu mwezi Januari yalikuwa hivyo siyo kwa sababu ya mwezi, bali kwa sababu yako wewe binafsi. Kwa kukosa mipango mizuri, au kwa kuwa na mipango ambayo siyo sahihi, umetengeneza matatizo kwenye maisha yako, ambayo umekuwa nayo kwa muda mrefu, na siyo tu mwezi januari. Hivyo basi, mwezi huu unaisha, lakini yale matatizo ambayo umekuwa unayatengeneza, utaendelea kuyatengeneza, kama hutachukua hatua kuyafanya maisha yako kuwa bora zaidi.

Habari nyingine za kusikitisha kuhusu mwezi Januari ni hizi, unakumbuka ile tarehe 31 disemba na tarehe 1 januari ulikuwa unaimba nini? Unakumbuka ulivyokuwa unasema mwaka mpya mambo mapya? Unakumbuka ulivyojiambia makubwa kwa mwaka huu 2018? Hebu sasa niambie unaendeleaje na yale makubwa uliyokuwa umeyapanga. Je bado unayafanyia kazi? Hivi hata unayakumbuka? Maana tafiti zimekuwa zinaonesha kwamba, baada ya wiki tatu za mwanzo wa mwaka, asilimia 90 ya watu wanakuwa wameshasahau malengo waliyojiwekea kwenye mwaka mpya, wanakuwa wamesharudi kwenye maisha ya mazoea.

Hivyo kama na wewe rafiki yangu, ulipanga makubwa mwaka huu ulipoanza, lakini sasa hivi mwezi wa kwanza tu ndiyo unaisha na hukumbuki hata ulijiahidi utafanya nini, mambo yako yataendelea kuwa magumu.

Swali ni je, unawezaje kuhakikisha maisha yako yanakuwa bora wakati wote? Unawezaje kuishi yale maisha ya mabadiliko unayoyataka? Unawezaje kuepuka baadhi ya miezi kuwa migumu sana kwenye maisha yako?

Na maswali yote hayo yana majibu sahihi, na majibu hayo yanaanza na kitu kimoja, tengeneza mfumo wa maisha yako, ambao utauishi kila siku, ije mvua, lije jua, wewe utaishi mfumo huo.

Watu wengi wamekuwa wanashindwa kwa sababu wanategemea hamasa. Wanahamasika na kuchukua hatua fulani, lakini kwa sababu hamasa huwa haidumu, basi wanajikuta baada ya muda wanaacha kufanya na wanarudi kwenye mazoea. Lakini kama utatengeneza mfumo bora wa maisha yako, ukaufuata mfumo huo, basi maisha yako yatakuwa bora wakati wote. Hakutakuwa na tofauti kwenye maisha yako, iwe ni Januari au juni.

Unapotengeneza mfumo wa maisha, unaangalia yale  maeneo muhimu sana kwenye maisha yako, ambayo unataka kupiga hatua. Yapo maeneo mengi, lakini mimi huwa napenda kuyagawa katika makundi matano muhimu. Makundi hayo ni maendeleo binafsi, kazi/biashara, fedha, afya na mahusiano.

Sasa huu ni mfano wa mfumo ambao unaweza kutengeneza na kuuishi kwenye maisha yako kila siku, na mfumo huu ukakuhakikishia unakuwa na maisha bora wakati wowote.

Maendeleo binafsi.

Kuwa na ndoto au maono makubwa ambayo unaishi kwa ajili ya kuyafikia. Kuwa na malengo na mipango ambayo unaifanyia kazi kila siku kwenye maisha yako. Halafu kila siku unapoamka, andika maono yako makubwa, pia andika malengo na mipango unayokwenda kufanyia kazi siku hiyo.

Andika vitu hivi kwenye kijitabu chako kila siku, na hii itaifanya akili yako kukuonesha fursa zinazoendana na kile unachotaka kufanya. Utaendelea kukumbuka maono yako makubwa, hata kama mambo yanaonekana kuwa magumu.

Kazi/ biashara.

Kama unafanya kazi, weka juhudi kubwa kwenye kazi hiyo, fanya kwa ubora wa hali ya juu sana, nenda hatua ya ziada kwa kufanya zaidi ya watu wanavyotegemea ufanye. Pia kazana kutoa thamani kubwa sana kwa chochote unachogusa.

Unahitaji kuwa na biashara, iwe una kazi au la, na kwenye biashara yako, kazana kutoa huduma bora kabia kwa wateja wako. Chagua tatizo ambalo linawasumbua watu, kisha weka juhudi kwenye kulitatua. Hakikisha maisha ya wengine yanakuwa bora wanapojihusisha na biashara yako.

Ishi kanuni hii muhimu sana ya kufikia uhuru wa kifedha kwenye maisha yako; mapato yawe makubwa kuliko matumizi, na kile kinachozidi, weka akiba na wekeza. Usikubali kabisa kutumia kila fedha unayoipata, utatengeneza matatizo. Hakikisha matumizi yako yanakuwa madogo kuliko kipato. Na hapa fanya vitu viwili, punguza matumizi na ongeza kipato.

Jilipe wewe mwenyewe kwanza, kwenye kila kipato unachoingiza, asilimia kumi usiitumie, hayo ni malipo yako, hupaswi kuyatumia kwa namna yoyote ile. Badala yake weka akiba na kisha wekeza ili izalishe zaidi.

Hakikisha unakuwa na mifereji mingi ya kipato, kipato chako kisitegemee eneo moja pekee. Kama umeajiriwa na unategemea ajira pekee kama njia ya kipato, umenasa kwenye mtego, kazana kujinasua kwa kuwa na mifereji mingine mingi ya kipato.

Mwisho kabisa kuhusu fedha, usikope kwa ajili ya kufanya sherehe, kula, kununua mavazi, kununua gari ya kutembelea, kujenga nyumba ya kuishi au kuanza biashara.

Afya ya mwili; kula vizuri, fanya mazoezi na pata muda wa kupumzika. Kila siku.

Afya ya akili; lisha akili yako chakula bora ambacho ni maarifa, soma vitabu, angalau kitabu kimoja kila mwezi, yaani kurasa 10 tu kila siku. Epuka habari hasi na za udaku, achana kabisa na habari zisizo na mchango wowote kwenye ukuaji na mafanikio yako.

Afya ya roho; Sali, tahajudi, kuwa mtu wa shukrani.

Kazana kuboresha mahusiano yako na wengine, hasa wale ambao ni wa muhimu sana kwako. Hapo unaanza na familia yako, unahitaji kutenga muda wa kuwa na familia yako, kusaidiana kwenye changamoto mbalimbali.

Pia boresha mahusiano yako na wengine wanaokuzunguka, kama wateja wako kwenye biashara, na hata jamii nzima unayoishi nayo.

Tengeneza mfumo wa kuishi kila siku kwenye maeneo hayo matano ya maisha yako, na hutakuwa na Januari ngumu kwenye maisha yako.

Rasilimali nilizokuandalia kuyafanya maisha yako kuwa bora mwezi Februari.

Karibuni Sana

By mr MIKAZI

Katika siku ya mwisho ya usajili : Arsenal kumsajili Aubameyang, Giroud kujiunga Chelsea na Batshuay kwenda Dortmund

Ikiwa dirisha la uhamisho linaenda ukingoni ambapo Adi kufikia saa tano usiku litakuwa limefungwa, leo kuna baadhi ya sajili zimefanyika ikiwa ni pamoja na Aubameyang kusajiliwa Arsenal,  Giroud kwenda Chelsea na Batshuay kujiunga na Dortmund. 

Bonyeza hapa kuendelea kusoma habari hii 👇👇

Taarifa za awali na Utabiri kabla ya mchezo kati ya Tottenham Hotspur dhidi ya Manchester united.

Leo kutakuwa na mtanange kati ya Tottenham Hotspur wakiwakaribisha Manchester united baada ya kufungwa goli 1 : 0 ndani ya Old Trafford mwaka Jana. Zifuatazo ni taarifa za awali za timu hizo mbili na utabiri kabla ya mchezo huo kuanza..hapo baadae
Bonyeza hapa ili uendelee kusoma habari hii 👇👇

Mashabiki Wa Manchester United :watoa ya moyoni kwa mkhitaryan kutokana na mechi ya Jana kati ya Arsenal na Swansea city

Mashabiki Wa Manchester united wamtolea ya moyoni mkhitaryan  kupitia mitandao ya kijamii kutokana na kauli yake aliyo isema baada ya kuhamia Arsenal kwamba Anaipenda Arsenal kwasababu inacheza mpira Wa kutafuta ushindi na sio kuzuia tu (kupaki basi) na hiyo ni baada ya Arsenal kuchezea kichapo cha 3 - 1 hapo Jana usiku. 

Bonyeza hapa ili kuendelea kusoma habari hii 👇👇

Swansea 3 - 1 Arsenal : Mambo matano yaliyo ongelewa

Katika mchezo uliochezwa Leo kati ya Swansea city na Arsenal  ambapo Mkhitaryan ndo kaanza rasmi kuitumikia Arsenal, Na mchezaji ambaye tayari amekwisha uzwa Giroud kushindwa kuiokoa Arsenal baada ya kuingia ikiwa Arsenal ipo nyuma kwa goli Moja. Kuna mambo matano yaliyo ongelewa kutokana na mchezo huu. 

Bonyeza hapa ili kuendelea kusoma habari hii 👇👇

matokeo ya mechi sita za mwisho ya Spurs na ya Man united

Matokeo ya mechi sita za mwisho ya Tottenham Hotspur na ya Manchester united huenda yana ashiria matokeo yatakayo patikana siku ya kesho ambapo Tottenham wanamkaribisha Manchester United. 

Bonyeza hapa ili kuona matokeo hayo 👇👇

Mambo sita yaliyo onekana katika uwanja Wa mazoezi Wa Arsenal

Mambo sita yaliyo onekana katika uwanja Wa mazoezi Wa Arsenal ikiwa Arsenal wanajiandaa kwa ajili ya mtanange dhidi ya Swansea katikati ya week hii ndani ya uwanja Wa Liberty (Liberty stadium). 

Soma hapa habari kamili 👇👇

Ya moto moto : Taarifa inayohusu sababu iliyofanya Spurs wakaribie kuchezea kichapo imetoka, Dele Ali ahusishwa

Michel Vorm, Eric Dier, Mousa Dembele na Dele Alli wahusishwa kuwa sababu moja wapo ya kutaka kupelekea Tottenham Hotspur kuchezea kichapo. 

Soma hapa habari kamili 👇👇

Arsenal wanakaribia kukubali

Arsenal wanakaribia kukubali kutoa kiasi cha kukaribia £60m kwaajili ya kumsajili Pierre Emerick Aubameyang kutokea Borussia Dortmund. 


Soma hapa habari kamili 👇👇

JE! wajua?

Kitendo cha kujikuta unafumba fumba macho bila kutarajia (eyes blinking) ukijumrisha kwa siku nzima inakadiriwa ni sawa na ku fumba macho kwa muda Wa dakika 30.


                          [Did you know]

TAHADHARI

*Picha hii haihusiani na tukio hilo*

Kuna mtindo mpya wa wizi umevamia Masherehe mbalimbali


Katika sherehe ya harusi ikiwa inaendelea majambazi uja na kuongea na MC wa harusi kuwa kuna gari namba fulani fulani nje ya ukumbi limezuia gari, hivyo MC utangaza na muhusika anapokuwa anatoka nje majambazi hao ujua hakika unakuja na funguo za gari hiyo hivyo unapofika kwenye gari wao huwa wapo na bastola na kukukamata na kukulazimisha kuendesha gari pamoja nao mpaka mbali na eneo hilo kisha          kuondoka na gari.

Ni vizuri kuwa mwangalifu juu ya hili, Zingatia mambo haya:


1. Usitoke muda huo huo unaposikia kuhitajika nje kusogeza gari.

2. Usitoke pekee yako, toka hata na watu wawili au zaidi.

3. Usielekee moja kwa kwenye gari lako, kwanza tazama kwa mbali kama kweli gari lako limezuia gari la mtu na hakikisha mtu yupo katika gari hilo na angalia kama kuna watu wengine eneo la gari lako.

*Kama hauna gari shirikisha wengine suala hili.*

Na hii ndio list ya Makipa na idadi ya michezo ya bila kufungwa katika EPL, De gea anaongoza

DE GEA kuongoza kwa kuwa na idadi nyingi ya kucheza bila kufungwa katika EPL

Ili kuona list hiyo ya makipa na idadi yao ya kucheza bila kufungwa bonyeza hapa 👇👇

Kilimo

Ukifanya kilimo cha kwanza kufahamu ni yafuatayo

1. Zao linaharibika ndani ya mda gani
2. Soko lako lipo kwa kiasi gani
3. Ushindani wa zao husika sokoni
4. Hali ya hewa na athari zake katika kilimo
5.Uwekezaji wenye tija wa kiasi cha pesa

Ifikie fursa, Itendee haki

Trump akutana na Kagame Davos

 January 26, 2018.Rais Kagame (Kushoto) na Rais Donald Trump wa Marekani wakutana mjini Davos, Uswizi. Ijumaa Januati 26, 2018.

Rais wa Marekani Donald Trump, Ijumaa alikutana na Rais wa Rwanda Paul Kagame na kumwita “rafiki” kufuatia maoni yenye utata anayodaiwa kutoa Trump kuhusu nchi za Afrika. .
Viongozi hao wawili walikutana mjini Davos, Uswizi, pembezoni mwa mkutano wa Baraza la Uchumi duniani ambao pia unahudhuriwa na viongozi na watu mashuhuri duniani.

Kagame alisema kuwa yeye na Trump walikuwa na “mazungumzo mazuri” juu ya masuala ya kibiashara na uchumi.

Rais huyo wa Marekani alimpongeza Kagame kwa kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa umoja wa Afrika wa mwaka wa 2018.

Kagame alimweleza Trump kwamba AU iko tayari kushirikiana na Marekani katika masuala mbalimbali..

Trump hivi karibuni alikosolewa na wengi kwenye mitandao ya kijamii na kwingineko baada ya ripoti kuibuka zilizodai kuwa alizitukana nchi za Kiafrika wakati akizungumzia suala la wahamiaji nchini Meru,

Hayo ni kwa mujibu wa wale waliokuwa katika mkutano. Hata hivyo rais amekanusha kutumia lugha ya matusi, lakini wale waliokuwa katika mkutano huo wamedai alifanya hivyo.

Kauli ya Trump ilipelekea kushutumiwa vikali na viongozi wa AU na baadhi ya viongozi wa nchi za Afrika kama vile Botswana na Ghana.
                                   [VOA]

IJUE SAFARI YA SÁNCHEZ KWA UFUPI ADI KUFIKIA USIKU HUU

Alexis Alejandro Sanchez Sanchez alizaliwa Mwezi Wa 12 tarehe 19 mwaka 1988, pia anajulikana kwa kifupi Kama Alexis, Ni mchezaji mwenye uzowefu kutoka Chile ambaye anacheza mbele Kama mshambuliaji katika klabu ya uingereza Manchester united na Chile katika timu ya taifa. Na ifuatayo ni historia yake kwa ufupi sana


                         Taarifa Binafsi


Jina kamili: Alexis Alejandro Sánchez Sánchez
Tarehe ya kuzaliwa: 19-12-1988

Mahali alipozaliwa: Tocopilla, Chile

Urefu: mita 1.6

Upande anao cheza: mbele (forward)au pembeni (winger)

                     Taarifa ya klabu


Timu yake ya sasa: Manchester united

Namba: 7

                  Timu ya vijana alocheza


2004-2005        :        Cobreloa

                    Timu ya wakubwa


Miaka.               Timu         Alicheza     Magoli 

2005-2006.     Cobreloa.    :     47              (9)
2006-2011        Udinese.    :    95              (20)
2006-2007  Colo-Colo (mkopo):  32            (5)
2007-2008  River Plate( mkopo):23           (4)
2011-2014.      Barcelona           :88          (39)
2014-2018.      Arsenal.            : 122          (60)
2018-    Manchester united.      :   1             (0)

                Kasababisha goli (1)

           

                          Timu ya taifa


2006-2008.     Chile chini ya 20 : 18.         (4)
2006-                  Chile                :  119       (39)


                           Mataji


                   Mwakilishi Wa chile


Mshindi.          Copa America.                   2015

Mshindi.        Copa America Centenario.    2016

Ameshiriki.      FIFA kombe la shirikisho.   2017

3.           FIFA chini ya 20 kombe la dunia  2007


                            [Wikipedia]