BADO HATMA YA SANCHEZ HAIJAFIKIWA

Manchester United na Arsenal kuendelea na majadiliano juu ya uwezekano wa mpango Wa kubadilishana wachezaji unaowahusisha Alexis Sanchez na Henrikh Mkhitaryan, hiyo ndio taarifa iliyowafikia Sky Sports.

Mkataba bado haujafikia muafaka kati ya pande zote mbili zinazohusishwa katika mpango huo, ikiwa ni pamoja na baadhi ya wawakilishi wanaohusishwa katika mpango huo.

Sky Sports News wanataarifa nyingine kwamba Arsenal wapo pia katika mazungumzo ya kumsajili mchezaji mwingine, inaaminika kuwa ni mchezaji Wa eneo la mbele la ushambuliaji Wa Borussia Dortmund ambae ni Pierre-Emerick Aubameyang.

Mkhitaryan yupo pamoja na kikosi cha united katika kiwanja Chao cha mazoezi cha Carrington Complex, baada ya kufika ijumaa asubuhi kabla ya kuikabiri hidi ya juu ya ijumaa asubuhi kabla ya kuikabiri Burnley mwishoni kwa wiki hii.
Bosi Wa united Mourinho alisema katika mkutano wake alioufanya leo ijumaa na waandishi wa habari: "Hakuna jipya. Ni wazi kila mtu anajua kwamba sisi tuna lengo la kumsajili Sanchez na hasa wakati meneja wa Arsenal alipoliongelea vizuri kabisa Kama alivyosema, hivyo hatuwezi kulificha hilo au kulikataa.

"Lakini mpango huo bado haujakamilika, haujakamilika kabisa. Katika wakati huu Mkhitaryan ni mchezaji wetu, Sanchez ni mchezaji Wa Arsenal. Na mechi ya kesho [jumamosi] nataka kuliweka swala hili pembeni na nizingatie swala la muhimu zaidi"

Mpango Wa Sanchez ya kuhamia Old Trafford inaeleweka kwamba inategemeana na mchezaji Wa kimataifa ambae ni mu Armenia Mkhitaryan kukubali masharti juu ya kuhamia Emirates.

Wakala Wa Mkhitaryan Mino Raiola aliithibitishia Sky Sports mapema wiki hii kwamba yeye alipendekeza ya mpango huo Wa kubadirishana zaidi ya wiki sita zilizopita.

Sanchez alikuwa piaakivutiwa na kujiunga na Manchester City, japo tayari Manchester city walijiondoa katika mazungumzo hayo,na pia wakati hivi karibuni Chelsea walionenekana kama wana nia ya kumuhitaji sanchez

Mkhitaryan amekuwa nje ya upendeleo ndani ya Old Trafford,alianza kipindi cha kwanza mchezo mmoja tu Wa ligi kuu kwa zaidi ya miezi miwili, na pia tatizo la kimkataba kwa Sanchez na Arsene Wenger limekuwa likijirudia mara kwa mara tatizo kwa zaidi ya miezi 12.

Sanchez mkataba wake unaishi msimu huu Wa majira ya joto, pamoja na mchezaji mwenzie Mesut Ozil, ambaye muda wake Wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo bado haujathibitishwa.

Wenger alisema wikiendi iliyopita alitarajia hatma ya baadaye ya sanchez kujulikana hivi karibuni.

                          [Sky sports]