Jose : Alexes hakuja kwasababu ya fedha

Jose Mourinho amedai sababu ya Alexis Sanchez kuamua kujiunga na Manchester United haihusiani na cha fedha.


Sanchez ilionekana angeweza kujiunga na Manchester City kabla hawajajiondoa katika mpango huo kutokana na gharama za mpango huo, na kuwaachia United kuingia katika mpango huo na kutoka kifua mbele.

Baada ya mourinho kuulizwa kwanini Sanchez alichagua kujiunga na United na sio City alisema "Sijui, ila nachojua Kama klabu nyingine zimeshindwa kumpata mchezaji, tatizo sio fedha kiukweli"

"We nenda na ukachambue idadi ya klabu na man cty, Chelsea hata Everton wametumia Fedha nyingi kuliko sisi.

"Inabidi uweke vitu katika mtazamo-ni kwa kiasi gani thamani ya Alexes Sanchez ingekuwa katika uhamisho Wa kawaida pamoja na miaka mitatu katika mkataba wake? angalia katika mahesabu ya haraka haraka ningekadiria kati ya £100m - £150m.

"Alexes angeenda popote pale, na alikuwa na sehem nyingi za kuchagua, Amechagua kuja hapa nafikiri mngemuuliza kwanini.

"Alikuwa ghali, alikuwa rahisi? Kiukweli mi nafikiri ili kuwa sawa kila upande (fair) ,nafikiri ni mpango mzuri saana kwetu"
Pep guardiola alisema waliamua kujiondoa katika mpango huo ili waendelee kutunza "uimara wao Wa klabu" lakini Mourinho alikuwa na mtazamo mwingine kuhusu hili.

Alisema "Sanchez ananikumbusha kidoogo msemo huu ukiuona mti na machungwa mazuri juu kabisa ya mti lakini hauwezi kuyafikia alafu unasema nimepata haya ya chini kwasababu sipendi Yale yanayo kuwa juu.

"Unayapenda Yale yanayokuwa kuwa juu, ni mazuri saana, ni machungwa kweli kweli, na yapo katika maduara mazuri, hivyo yana juisi ya kutosha ,lakini huwezi kuyafikia.

"Kwahiyo lazima utasema sikutaka kwenda juu au nayapenda haya ya chini. Nafikiri imenikumbusha kidoogo kuhusu hiyo simulizi"

                            [Sky sports]