JE, UNAJUA KWANINI NDOTO YAKO YA KUWA NA MAFANIKIO MAKUBWA INAZIDI KUYEYUKA?

Je, unajua kwanini ndoto yako ya kuwa na mafanikio makubwa inazidi kuyeyuka kadri siku zinavyozidi kwenda ? kiukweli sio kazi rahisi. Lakini wakati huo huo, mabadiriko unayoweza kuyafanya katika maisha yako ili utimize ndoto zako Ni marahisi . Ni maraahisi, lakini si mepesi. Na yote yapo katika akili yako. Je, uko tayari kufanya mabadiliko makubwa katika maisha yako? Twende pamoja tukaangalie sababu 13 za kwanini wewe kamwe hauta kuwa ni mwenye mafanikio katika maisha yako. 


1. Kujiweka mbali na majukumu (kuyaogopa majukumu)

Wajibika ipasavyo katika kila kitu kinachotokea ndani ya maisha yako ya kila siku.usiwalaumu watu wengine, Usilaumu kwa chochote kinachoweza kujitokeza, usilaumu kwa vitu ambavyo unavikosa, usilaumu kwa matokeo ambayo unayapata.Daima utakuwa na maamuzi ya kuchagua kitu cha kufanya katika kila hali,na maamuzi hayo daima yatakuwa na matokeo (hasi au chanya) .

Lichukuwe jukumu na ufanye maamuzi sahihi, kwasababu maamuzi hayo huenda yakakupeleka karibu kabisa na kuyafikia malengo yako au kukupeleka mbali zaidi.Mafanikio sio kitu kingine ila Ni mfululizo Wa maamuzi yote sahihi unayochagua kuyafanya. Kama unataka kitu, nenda ukipate mwenyewe .Wewe ndio kiongozi Wa mafanikio yako.AMKA

Mimi ni bwana wa hatma yangu, mimi ni nahodha wa nafsi yangu. ~ William Ernest Henley


2.mchelewaji Wa kufanya maamuzi


Elewa athari za kuwa mchelewaji Wa kufanya maamuzi. Ni kama kadi ya benki .ukiwa nayo unafanya starehe mbali mbali za kukupa furaha huku unasubiri uletewe muswada Wa malipo (bill) ya matumizi yako.uchelewaji Wa kuamua Ni sawa na kuwa mfu alie hai.

Mimi sijali Kama kuna sababu zinazokufanya uchelewe kuamua. Sheria ya Utovu Wa Dhamira inasema kwamba kama haujachukuwa hatua Mara baada ya kupata wazo flani na wakati huo ndio ulikuwa ukiliwazia Sana hilo swala,basi haraka haraka wazo hilo litaanza kupotea na kadri unavyoendelea kusubiri ndivyo utakavyoshindwa kufanikisha mpango wako.

Anza upya kwa kufanya uamuzi wa kutangaza vita dhidi ya Imani mbaya ya kuchelewa kuamua na huku ukiendelea kuwa na ufahamu kwamba wewe Una haja ya kutoacha vita hii (ya kuchelewa kuamua) dhidi ya shetani, kuanzia hapo wewe Ni tayari uko mbele ya wengi.

Uchelewaji Wa kuamua ni moja ya ugonjwa unao wapata wengi na Ni ugonjwa hatari saana. Na madhara yake makubwa Ni kuto fanikiwa na kuisahau furaha kabisa ~ Wayne Gretzky

3.Unataka kila kitu kiwe kimekamilika(kiwe sawa) 


Ukamilifu haupo duniani.fanya kwa uwezo wako wote; pambana ufanye vizuri ; pambana uwe zaidi ya ulivyokuwa Jana ; ila sahau kuhusu ukamilifu,kwasababu Kama kazi yako ni kufanya kila kitu kiwe katika ukamilifu unaoutaka, kamwe hautaweza kufikia kiwango icho hata ufanyaje.

Na acha kusubiri wakati mzuri au mpango bora ,kamwe hautatokea,Na Kama ukitokea, ujue utazunguka tu na hatimae utaishia njia panda. Unachotakiwa ni kuanza leo, uendelee kesho na siku zinazofuata.

Ndoto yako kamwe haiwezi kuja kuzaa matunda kama wewe kazi yako ni kuandaa na kusubiri tu.itatimia endapo utafanya na kuchukuwa hatua kubwa.

Usisubiri, kwani hautaweza pata wakati sahihi. Anza hapo hapo ulipo, haijalishi unaanza na vifaa vya aina gani (katika hali gani) na vifaa vizuri utavipata mbele ya safari kadri unavyozidi kufanikiwa~Napoleon Hill

4.Unaogopa kukosolewa


Ukiwa unaelekea kwenye kufanikiwa katika kitu chochote, tarajia kukutana na watu watakao kukosoa na kukuchukia ,jifunze kukabiliana nao, Jifunze aina ya ukosoaji unaoweza kuupokea na aina ya ukosoaji ambao unatakiwa ujiepushe nao. Sio kila aina ya ukosoaji ni Wa kuufanyia kazi.

Katika mazingira yoyote,usiruhusu kuwa na hofu ya kukosolewa ikakufanya uache kile ambacho unatakiwa kufanya, hautakiwi kumsikiliza kila mtu, ukifanya hivyo unajitengenezea njia ya kutofikia malengo. Hayo ni malengo yako, Kwa ajili ya maisha yako, Amua kufanya .

Ukitaka usikosolewe basi, usiseme lolote, usifanye lolote, ili uwe mtu usio na chochote. ~ Aristotle

5. Unaogopa kushindwa(kufeli) 


Fanya mambo kwa ajili ya mafanikio, lakini tarajia pia unaweza kushindwa njiani. Kushindwa ni muhimu kabisa. Kushindwa ni somo la maisha ambalo lipo ili likujenge uwe mtu bora zaidi. Kama wewe una hofu ya kushindwa, basi usianze kufanya.
Ni sawa kuwa na hofu kiasi , lakini kushindwa kusikufanye ukate tamaa Kwa sababu si juu tu ya Mara ngapi unaanguka au kwa kiasi gani unaanguka, ila tu ni jinsi gani unainuka baada ya kuanguka na kujaribu tena na tena.

Ni vigumu kuishi bila kushindwa katika kitu,labda ukiishi kwa uangalifu Wa hali ya juu kitu ambacho huwezi kuishi katika maisha yako yote na katika hali hiyo a, unaweza jikuta unashindwa bila kujua sababu. ~ J. K. Rowling

6. Ni mvivu Wa kupita kiasi


Kama wewe huwezi kufanya kazi flani adi awepo mtu Wa kukusimamia au kukuangalia basi jijue wewe ni mvivu., hii ni dunia ya ushindani, Kama unataka kushinda basi inabidi ujiandae kiakili na ufanye kazi kwa bidii mara mbili zaidi ya mtu mwingine. Kama wengine wanafanya kazi masaa matano, wewe fanya masaa saba, fanya kazi kwa nguvu zote,utafanikiwa . Na sahau mambo yote kuhusu kwenda kustarehe.

Kanuni ya mafanikio: kuamka mapema, kufanya kazi kwa bidii, kataa vitu vya mteremko. ~ J. Paul Getty

7. Unakosa uhalisia na ubunifu


Wewe tayari ni mvivu kama hauongezi chochote yaani unafanya kitu Kama watu wengine wanavyofanya .Una haja kubwa ya kuwa wakipekee Kama unahitaji kuibuka mshindi.
thubutu kuwa Wa tofauti katika kundi la watu na Unaweza kupata mawazo na msukumo kutoka kwa watu wengine,pia Unaweza hata kwa kiasi flani uka iga kutoka kwa wengine Lakini mwishoni kuwa wewe Kama wewe na Watu wanapenda kuona unafanya kitu cha tofauti na sio unafanya kitu cha kuiga.

Ku uamini utofauti wako na watu wengine unakupima jinsi ya kujua kujitegemea ~ James Broughton


8. Unafanya kila kitu wewe


Sisi binadamu Ki baiologia tumeumbwa kutegemeana. Mafanikio hayawezi kuletwa na wewe mwenyewe tu,
Usiogope kuomba msaada Kama ukiuhitaji, jifunze kwa kipekee kujuana na watu wengine na mfanye kazi kwa pamoja ,mpeane nguvu, wasaidie na wathamini wengine, usitegemee kupokea ikiwa wewe hautoi

Anza kwa Kukutana na watu, kukaa nao pamoja ikiwa ni muendelezo na kufanya kazi pamoja ni mafanikio ~ Henry Ford

9. Hauna shukrani 


Kuwa na shukrani kunaongeza kiwango cha furaha yako kwa kiasi kikubwa. Wewe utakuwa bora zaidi kutatua changamoto unazokutana nazo katika maisha Kama muda mwingi utakuwa ni mwenye matumaini, furaha, na mwenye kushukuru. Furaha inapelekea kuwa ni mwenye kufanikiwa na Si vinginevyo.

Anza kujijengea tabia ya kuwa ni mwenye kushukuru na ikiwezekana kuwa ni mwenye kushukuru, Iache shukran itawale maisha yako. Angalia mazingira yalioyo kunzunguka ukiwa unasoma ujumbe huu. Bila Shaka kutakuwa na jambo angalau moja litakufanya maisha yako kuwa tofauti saana Kama ulishapotea. Na usifanye makosa, huu sio wakati Wa wewe kukaa tu na kile ulicho nacho na kushukuru bali shukuru na endelea kufanya.

Kuendeleza tabia ya shukrani, na kutoa shukrani kwa kila kitu kinachotokea katika maisha yako, huku ukijua kwamba kila hatua unayoipiga ni hatua ya kuelekea kwenye mafanikio ni bora zaidi kuliko hali yako ya sasa. ~ Brian Tracy

10. Unashimdwa kujifunza kutokana na makosa yako


Ukiwa Njiani kuelekea kwenye mafanikio, utajikuta ukifanya makosa mengi saana, yakubari makosa hayo kwa unyenyekevu kwa maana hayo makosa ni baadhi ya mafunzo ya bure unayoyapata katika maisha. Lipokee kila kosa unalolifanya Kama limekuja kukufundisha kitu cha muhimu zaidi na cha lazima kukijua ili uweze kufikia mafanikio yako katika siku za mbeleni.

Einstein amesema kwamba maana ya kuchanganyikiwa (uchizi) ni kufanya kitu kimoja tena na tena na kutarajia matokeo tofauti. Kujifunza kutokana na makosa yako na kufanya bila kuyarudia.

Kujifunza kutokana na makosa yako ni ujuzi muhimu ambao unakuwezesha wewe kuwa na ujasiri na kuwa kiongozi wa mabadiliko badala ya kuwa ni mwathirika wa mabadiliko. ~ Brian Tracy

11. Haujiamini


 Jitoe katika fikra potofu (imani) ya kusema huwezi. Kama unataka kitu kwa nguvu na Nia ya dhati , lazima utapata njia ya kufanya lisilowezekana kuwezekana. Fikra potofu za kusema huwezi, zipo katika akili yako mwenyewe hivyo basi unaweza ukazibadirisha.

Wewe hakuna anaeweza kukuzuia .kuwa na Ndoto kubwa kwa sababu umeumbwa kufanya mambo makubwa na amini kwamba utakuwa na mafanikio makubwa, Wewe tayari una kila kitu cha kukufanya uyashinde maisha kilichobaki ni kifanikisha tu.

Kama matamanio yako ya kufikia malengo yana nguvu ya kutosha, utajikuta Una nguvu za ajabu za kukuwezesha kufikia malengo hayo. ~ Napoleon Hill

12. Hauna msimamo


Kuwa na 'msimamo' ni muhimu katika mafanikio yako. Endeleza tabia ya kufanya jambo wakati wote, haijalishi wakati huo unajisikia kufanya hilo jambo au laa. Mtu anaetaka kufanikiwa hajitaftii sababu za kutofanya (udhuru) jambo. Yeye huwa anahakikisha jambo hilo linafanyika. Sababu za mpito haziwezi kumfanya asifanikishe jambo hilo.
Jitengenezee mfumo mzima Wa maisha yako na hakikisha unaufuata ipasavyo. Mfano, Kuamua na kufanikiwa kufanya mazoezi mara nne kwa wiki ni bora zaidi kuliko kuamua kufanya mazoezi mara saba kwa wiki na kushindwa kutekeleza hata mara tatu. Ndiyo, hata matokeo yake yanafanana, kwa sababu unajitengenezea udhaifu katika akili yako mwenyewe kwa kutofanya kile unachosema utafanya. Huo udhaifu Wa kutokuwa na msimamo kwa muda mrefu utaishia kujikuta haufiki popote daima.

Sisi tulivyo sasa ni sababu ya vile tulivyokuwa tunarudia kufanya. Ubora, Wa mtu, si kutenda, bali kuwa na tabia ya kutenda. ~ Aristotle

13. Umeacha kujiendeleza


Watu waliofanikiwa
wanaelewa kwamba wana haja ya kuongeza ujuzi wao wakati wote. Huwa wanaelewa kwamba mara baada ya kuacha ,watakuwa nyuma katika ushindani. Waliweza kufanya maamuzi mapema ya kuingia katika ushindani Wa kuwa bora katika vitengo vyao (fani zao).

Wakati ambao unaacha kujiendeleza zaidi ndio wakati ambao unajipelekea kushindwa. Hiyo ni pamoja na kujiendeleza kwa wewe kama wewe (kitaluma au ujuzi) na mazingira yote yanayozunguka maisha yako (unapoishi, unapofanyia kazi na n.k) . Ki ukweli, wakati ambao utaona ulipofikia panatosha apo ndipo utakuwa ni mwenye kushindwa maisha.

Hatua yako ya mafanikio itakuwa mara chache zaidi ya hatua yako ya maendeleo binafsi. ~ Jim Rohn

Nakutakia kila la heri katika safari yako ya mafanikio


                         [life hack]