KIJANA WA SASA NA KAZI


BILA SHAKA KAZI NI MUHIMILI MKUBWA WA MAENDELEO KWA WATU WOTE KATIKA NCHI.
ila kwa asilimia kubwa changamoto ya kupata kazi katika sekta rasmi nayo imezidi kuongezeka hasa kwa kuwa na ufinyu wanfasi hizo kwa miaka ya karibuni
swali la kujiuliza lenye msingi mkubwa
je kijana awezaje kujipatia kipato katika sekta zisizo rasmi (ujasiriamali, kilimo, makampuni binafsi, utalii n.k)

majibu ya swali hili laweza kuwa mengi, ila amini kijana unayetafuta kazi ama kuanza shughuli binafsi wewe mwenyewe ndiye nguzo ya kujiinua

jichanganye na watu, eleza shida yako kwa watu ili upate upenyo na zaidi ya yote jitahidi kwa kadiri uwezavyo kutokata tamaa, ongeza bidii katika kutafuta kazi, funga na kuomba, ila zaidi kuwa mbunifu katika kufanya kazi binafsi hasa ujasiria mali, jitolee kwa makampuni nawe itakuwa rahisi kupata kazi.