CHELSEA wamesimamisha maongezi kwa muda juu ya kuwasajili wachezaji wawili kutokea ROMA

Chelsea wamesimamisha maongezi kwa muda juu ya kuwasajili wachezaji wawili Wa Roma ambao Emerson na Edin Džeko. 


Chelsea kuendeleza mazungumzo zaidi na Roma juu ya uwezo wa kuwasajili wachezaji wawili wiki ijayo ambao ni Emerson Palmieri na Edin Džeko .

 Wanamatumaini kwamba Palmieri atakuwa akicheza nyuma upande Wa kushoto akisaidiana na Marcos Alonso endapo watakamlisha mpango Wa kumsajili na kutua ndani ya Stamford Bridge , licha ya ukweli kwamba Chelsea wanaweza kumchukuwa mbrazil huyo kwa mkopo.

Roma wanataka £milioni 22 kwa ajili ya Palmieri, lakini kuna matumaini kwa pande zote kuwa mpango huo unaweza kamilika kwa mkopo au uhamisho Wa kudumu.


Chelsea wanania ya kumuhitaji Džeko japo baado hawaja fika mbali kimazungumzo na lengo hilo lilikuja baada ya klabu kumuhitaji mtu atakae msaidia Morata,ambae ana adhabu ya kuto kucheza mechi ya jumamosi ambapo Chelsea watasafiri kimchezo kuelekea Brighton.

Edin Dezeko akifunga goli lake la pili katika magoli mawili aliyo yafunga katika sare ya 3 : 3 na Chelsea walivyo chuana vikali mwezi Wa kumi mwaka kaja


Anae msaidiaga Morata kwa maana Michy Batshuayi, ambaye anaweza kuwa katika mpango Wa kubadirishana wachezaji kati ya yeye na Džeko, anatarajiwa kuanza dhidi ya Brighton. Na Roma watakutana uso kwa uso na nter Milan siku ya jumapili,kwahiyo Ina maanisha majadiliano hayo yamesimamishwa kwa muda mwishoni mwa wiki hii.

Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu walikuwa na matumaini ya kumsajili Andy Carroll, lakini mchezaji huyo Wa West Ham United ambae anacheza mbele upande Wa katikati ameumia kifundo cha mguu ambapo inawalazimisha Chelsea kuangalia mahali pengine. Ila kuna matumaini Chelsea wakarudisha Nia yao kwa mchezaji huyo mwenye umri Wa miaka 29 Kama atapona mwishoni kwa mwezi huu.

                             [Telegraph]