
Kufuatia msimu na nusu ya moto na baridi(kiangazi), Mourinho kwa sasa anafuraha kumuachia Mkhitaryan aende, kutokana na kutokuona kwa kile kiwango chake bora muda mrefu. Je Ni kosa la Mourinho? Kwa nini Arsene Wenger anafikiri bado mkhitaryan anaweza kufanya vizuri zaidi?
Hebu tuangalie hapa.
Mfumo unao mfaa
Mfumo mama Wa Mourinho hauruhusu mchezaji kupata muda Wa kuwa huru kuonesha ubunifu wake, kitu ambacho Mkhitaryan amekuwa akikifanya katika klabu alizopitia. Alipokuwa Chini ya Jurgen Klopp yeye zaidi alikuwa Kama namba 10 yaani alicheza katika safu ya kushambulia , wakati Thomas Tuchel, alipokuwa meneja katika msimu wa 2015/16 Mkhitaryan alifunga magoli 11 ya ligi kuu na kusaidia (assist) 15, kutumika Kama mshambuliaji Wa ndani upande Wa kushoto ambapo ni sawa na alichofanya aliekuwa kabla yake.
Ndani ya Arsenal, Wenger ni Kama anataka kumuweka mkhitarian katika nafasi ya zamani ya Sanchez kama mshambuliaji Wa upande Wa kushoto mbele namba 10 kakita mfumo wao Wa sasa 3-4-3
[Telegraph]