Rais wa Marekani Donald Trump, Ijumaa alikutana na Rais wa Rwanda Paul Kagame na kumwita “rafiki” kufuatia maoni yenye utata anayodaiwa kutoa Trump kuhusu nchi za Afrika. .
Viongozi hao wawili walikutana mjini Davos, Uswizi, pembezoni mwa mkutano wa Baraza la Uchumi duniani ambao pia unahudhuriwa na viongozi na watu mashuhuri duniani.
Kagame alisema kuwa yeye na Trump walikuwa na “mazungumzo mazuri” juu ya masuala ya kibiashara na uchumi.
Rais huyo wa Marekani alimpongeza Kagame kwa kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa umoja wa Afrika wa mwaka wa 2018.
Kagame alimweleza Trump kwamba AU iko tayari kushirikiana na Marekani katika masuala mbalimbali..
Trump hivi karibuni alikosolewa na wengi kwenye mitandao ya kijamii na kwingineko baada ya ripoti kuibuka zilizodai kuwa alizitukana nchi za Kiafrika wakati akizungumzia suala la wahamiaji nchini Meru,
Hayo ni kwa mujibu wa wale waliokuwa katika mkutano. Hata hivyo rais amekanusha kutumia lugha ya matusi, lakini wale waliokuwa katika mkutano huo wamedai alifanya hivyo.
Kauli ya Trump ilipelekea kushutumiwa vikali na viongozi wa AU na baadhi ya viongozi wa nchi za Afrika kama vile Botswana na Ghana.
[VOA]