ARSENE WENGER KAMTOLEA UVIVU SANCHEZ

Arsene Wenger kamtolea uvivu Alexis Sanchez na kusisitiza kuwa Sanchez kaiacha Arsenal na kujiunga na Manchester United kwa ajili ya fedha


Wenger amedai kwamba "katika miaka 30 ya kufanya uhamisho nimejifunza mengi kuhusu binadamu" baada ya kuongea  kuhusu Sanchez ya kuondoka

Arsene Wenger amesisitiza Alexis Sanchez kahamia Manchester United  yote ni sababu ya fedha.

Bosi Wa Gunners  Wenger alidai  Sanchez kwenda Old Trafford kwa ajili ya kutaka  mkataba wake Wa kumalizia kazi yake uwe ni Wa fedha nyingi zaidi na ni kweli ndomanda hata Manchester city walishindwa kulimudu hilo na hiyo ni ishara tosha ya kuthibitisha hilo.

Sanchez ameondoka Arsenal kwa ajili ya fedha £400,000--kwa wiki, na kasainiwa kwa Ada ya £15m na miaka take minne na nusu ya mkataba itamfanya kuwa mchezaje alielipwa pesa nyingi saana katika ligi kuu.
Wenger alisema: "siwezi kumuelewa mtu yeyote anaetaka kuondoka Arsenal. Lakini katika miaka 30 ya kufanya uhamisho  nimefunza mengi kuhusu binadamu.

"Kama mtaalamu (professional Player), ilikuwa labda ndo mkataba wake Wa mwisho katika ngazi ya juu na ni Wa muhimu. Baada ya hilo, Mimi nimelikubali (la uhamisho Wa sanchez) kwa sababu sisi tulilikubali kwamba tutamuachia aende. Baada ya kuchambua faida na hasara. "
Sanchez  akiwaaga kwa kuwapungia Arsenal baada ya kulikubali dili kubwa la kuhamia man utd

"Sisi tulifanya kile tulichojaribu kukifanya na tulienda mbali Adi pale tulipoweza t. Hata Manchester City walienda na mwishoni wakashindwa.na hiyo Ina maanisha kwamba hatukupata nafasi ya kumpa mkataba mpya."

Maneno ya Wenger yalifanya kila kitu kieleweke wazi alichofikiria kuhusu Sanchez kuondoka Arsenal ila Bosi huyo Wa Arsenal alisisitiza watakuwa imara kupitia upande nyingine.

Arsenal wanajiandaa kukamilisha mpango Wa Henrik Mkhitaryan kujiunga kutoka Manchester United na mchezaji Wa Borussia Dortmund  Pierre-Emerick Aubameyang inatarajiwa kufuata.

                            [Mirror]