David de Gea amekataa kuhusishwa na uvumi kwamba yeye hivi karibuni ataingia mkataba mpya na Manchester United , lakini ameelezea furaha yake kuwa katika klabu ya kipekee saana.
Mlinda mlango huyo mwene umri Wa miaka 27 mkataba wake Wa kuitumikia Manchester united unamalizika ifikapo mwisho wa msimu ujao na kuna uvumi kwamba yupo kwenye mazungumzo ya kuingia mkataba mpya Wa muda mrefu zaidi kuweka kuanza zaidi Old Trafford.Alipoulizwa kuhusu mkataba wake katika mahojiano maalum na Sky Sports, De Gea alisema: "sidhani kama ni wakati wa kuanza kuzungumza juu ya siku zijazo, na si wakati wa kukaa na kuzungumzia mikataba.
"Tuna michezo kati ya sasa na mwisho wa msimu na jambo la kwanza kabisa kufikiria Ni kuhusu mechi yetu na Burnley mwishoni mwa wiki hii.
"Ni yote kuhusu kutuliza kichwa, kuwa na malengo, kufanya kazi kwa bidii, kushinda katika mazoezi, kujiweka imara na kuokota pointi."
Wakati De Gea alikuwa akisita kujadili mustakabali wake, yeye hakusita kusema furaha anayoisikia kwa kuwepo Manchester United.
"Tu kuwa sehemu ya klabu hii ni maalum ambayo Ni yakipekee yenyewe," alisema. "Kuwa mchezaji na sehemu ya klabu hii maalum, na kupata nafasi ya kuvaa jezi, na kwenda mbali kwenye mechi, ni kitu ambacho daima kitakuwa fahari na maalum sana.
"Kuwa sehemu ya klabu kubwa kama Manchester United inakufanya uwe na hisia na taratibu unatambua jinsi gani ya klabu Ina maana kwa mashabiki na watu ambao wanafanya kazi hapa. Kwakua wanaishi kwa ajili ya mechi, hivyo kwamba wanakuwa sehemu ya wewe na unaweza tu kufahamu kwamba uliutumia muda wako hapa"
De Gea amekuwa Wa Ki maajabu katika kipindi cha msimu huu akiwa chini ya meneja Jose Mourinho akisema yeye ni "kipa bora katika dunia" baada ya kuokoa mikwaju kadhaa ya hatari na kushinda 3-1 dhidi Arsenal mnamo mwezi desemba 2017
.Alipoulizwa juu ya uwezo wake Wa kulinda lango , De Gea alisema kwamba hiyo yote Ni kwasababu ya aliekuwa mshauri Wa zamani Wa Atletico Madrid bwana Emilio Alvarez ambaye Ni kocha Wa makipa Wa Manchester united.
"Sisi tulijuana tokea muda mrefu na kufanya kazi kwa pamoja tangu nikiwa kijana mdgo Sana " De Gea alisema. "Yeye anajua nini cha kunambia, jinsi ya kukabiliana na mimi kama kuna mashaka yoyote yakiingia katika akili yangu, yeye amenisaidia mambo mengi ya kutisha.
"Yeye anajua mimi kama mchezaji na kama mtu na kuna hisia maalum ambayo ipo kati yetu, na kwa kweli tuna uhusiano mzuri saana Wa kikazi, hivyo nadhani kama wewe ukijiuliza juu ya sababu ya mambo kwenda vizuri msimu huu hii inaweza kuwa Ni kutokana na moja ya sababu ya nyuma yake."
Licha ya De Gea ya kuwa na kiwango kizuri cha kulinda goli, United bado wanajikuta pointi 12 nyuma ya wanao ongoza Ligi Kuu Manchester City.
De Gea anasema itakuwa "vigumu" kuwakamata man cty, lakini si vigumu.
"Kiukweli unaweza kusema ni vigumu, lakini katika Ligi Kuu huwezi kujua nini kitatokea," alisema.
"Ni vigumu sana katika ligi ya ushindani . Ni wazi itakuwa ngumu. Kuna kabisa pengo kubwa, pointi 12 ni nyingi, lakini sisi tutapambana kwa nguvu zetu zote katika kila mchezo ili tupate pointi nyingi naamini tunaweza na kisha tuone ambapo sisi tutaishia katika mwisho wa msimu. Hakuna kukata tamaa ni kupambana mpaka mwisho."
[Sky sport]