MORATA na FABREGAS nje ya msafara

Chelsea katika jumatano ya kesho itakuwa bila ya Alvaro Morata na Cesc Fabregas katika nusu fainali ya pili ya kombe la Carabao ambapo watachuana na Arsenal. 


Nusu fainali hiyo ya pili ni baada ya draw 0-0 katika mechi ya kwanza ndani ya uwanja wa Stamford Bridge lakini Chelsea itakuwa bila watu hao wawili muhimu katika mchezo huo Wa marudiano.

Hata hivyo, beki kuhusu Andreas Christensen imewekwa wazi kuwa atacheza, licha ya kufanyiwa mabadirisho katika mechi iliyochezwa  mwishoni mwa wiki iliyopita kutokana na kuumia kichwa.

Conte amesema: "Morata na Fabregas wapo nje,  hawata kuwepo katika mchezo dhidi ya  Arsenal. 
"Morata Ana tatizo katika mgongo,"

" hivyo natakiwa niangalie na hali halisi kabla ya kufanya uamuzi mzuri (Wa kuchagua watakao cheza) "

Na kuhusu Manchester city ambao ndio wanao ongoza ligi Conte amesema, kuna hamasa kubwa katika klabu za London katika michuano ya usiku Wa jumatano .

"Kwa Mimi na wachezaji, ni shabaha ya muhimu Sana (muhimu kushinda) " Amesema Conte. 

" katika msimu wangu Wa kwanza na nusu,  Nina nafasi ya kushinda ligi kuu, kucheza fainali ya FA cup na kucheza (Community shield) ngao ya jamii ."

"Sasa hivi nna nafasi nyingine ya kucheza fainali ya Carabao cup (kombe LA Carabao) ."

"Kwa maana hiyo Nina michezo miwili ili nitinge fainali, baada ya kutoka sare ya 0 : 0, na hakika mchezo utakuwa Wa wazi saana"

Arsena wamemuuza Sanchez na walie msajili ambae ni mkhitaryan haruhusiwi kucheza mchezo huo lakini Conte hana Imani kuwa Gunners watakuwa wadhahifu kiasi hicho. 

"Nafikiri Arsenal,  wanakikosi kizuri na sioni nafasi yoyote ya kunifanya niwezi kushinda mchezo huo" alisema Conte 

"Kucheza dhidi ya Arsenal siku zote ni mtihani mkubwa"

                             [Sky sports]