MOURA: Sina furaha ndani ya PSG

Lucas Moura amesema Hana furaha ndani ya  Paris Saint-Germain (PSG)  baada ya kuendelea kuwekwa nje (benchi) ya kikosi katika klabu hiyo ya daraja la kwanza. 

Moura ameonekana katika mechi sita tu msimu huu ndani ya PSG, ambao wanaeleweka Kama wanasikilizia klabu zitakazo hitaji kumnunua mchezaji huyo mwenye umri Wa miaka 25.

Vyanzo vya habari vya karibu na winga huyo vili iambia Sky Sports News kwamba Tottenham wana Nia ya kumchukuwa Moura, wakati Manchester United walikuwa na nia  katika siku za nyuma.

Moura awali aligusia kwamba anatarajia kuondoka kuelekea katika Ligi Kuu ya uingereza na Brazil kimataifa, aliiambia L'Equipe yeye anaganda na baridi kutokana a kuwekwa benchi na timu hiyo ya kifaransa kwa muda mrefu.

"Ni pigo la kikatili," alisema. "Mimi nina ganda tu kwasababu sipewi tena nafasi ya kucheza, na tena kuwa na uwezo wa kuonyesha uwezo wangu  kama nilivyokuwa nikifanya hapo awali.

"Mimi sina furaha. Nilidhani ningejengwa na kuwa imara na klabu hii, lakini hilo liko wazi kwamba sio lengo lao."

Moura, ambae alihamia PSG kutokea Sao Paulo mwaka 2013, bado Hana uhakika juu ya  hatma yake ya mbeleni lakini anadhani mtindo wake Wa kucheza unaweza kuwa ni wenye kufaa zaidi ndani ya Hispania.

"Ni kweli kwamba La Liga inaweza kunifaa ," aliongeza. "Na kasi yangu na mbinu, mimi naweza kufanya vizuri huko.

"Lakini haijarishi wapi nitakapo elekea, mimi najua kile ambacho nina uwezo nacho. Sijakuwa Wa kimataifa kwa kubahatisha".

                            [Sky sports]