Arsene Wenger amethibitisha mpango wao Wa uhamisho kati yao na Manchester United unaowashirikisha Alexis Sanchez na Henrikh Mkhitaryan bado unaweza kutokea januari hii
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amesema AlexisSanchez kuhamia Manchester United ni "inaweza kutokea" katika masaa 24 ijayo
Wenger pia alisema "kumlipa mshahara Henrikh Mkhitaryan haitakuwa tatizo" na hiyo ilikuwa Ni kuhusu mpango Wa kubadirishana wachezaji Alex na mkhitaryan na muarmeni huyo anaonekana ndo anaenda kuziba pengo la Alex, na kuhusu Mesut Ozil "hataondoka katika klabu januari hii" alisisitiza.
"Nimekuwa katika kazi ya uhamisho (transfer) kwa muda wa miaka 30 hivyo huwa inatokea wakati wowote mambo yanaweza kuwa tofauti," Wenger alisema.
"Hivyo ndivyo soko la uhamisho(transfer market) linavyokuwa ,ila cha muhimu Ni kwamba isizidi mipaka hivyo hatuna budi kukubali kwamba kinaweza pia kutokea chochote. Mambo ya aina hii huwa hayatabiriki kamwe ."
Alipoulizwa kama Mkhitaryan alihusika katika mpango huo, Wenger alisema: "uelewa Wangu ni ndiyo. Na kuhusu kumlipa Mshahara haiwez kuwa tatizo"
bila shaka [natamani awe kwenye kikosi changu].na huu mpango umewezekana ni kwa sababu mimi natamani niwe na mchezaji (mikhtarian) kwenye kikosi changu.
"Tulicheza mara nyingi dhidi yake wakati yeye alikuwa katika Dortmund hivyo yeye bila ya shaka alitokea kuvutiwa na ubora wa michezo yetu na aina ya mchezo sisi tunaocheza hivyo Ni kwamba bila ya shaka yeye anapenda klabu.
"Hii itakuwa kubadilishana kati ya wachezaji na nadhani mtu anaweza kuchukua nafasi nyingine sio lazima acheze nafasi ya aliabadirishwa nae. Je Sisi bado tupo katika soko la uhamisho sbaada ya hapo? Ndiyo."
Manchester United wako tayari kulipa Alexis Sanchez zaidi ya us $ 350,000 kwa wiki na Wenger ameweka wazi Arsenal "clabu ilijitahidi kwa kadri ya uwezo wake Wa hali ya juu" ili Alex abaki.
[Sky sport]