Alexis Sanchez aliukosa mchezo Wa Ligi Kuu ambapo Arsenal iliibuka na ushindi dhidi ya Crystal Palace kwasababu alikuwa safarini kuelekea kaskazini kujadili kuhusu uhamisho wake Wa kwenda Manchester United, alisema Arsene Wenger .
"Sikuweza kumpanga kwenye kikosi kwa sababu kuna suala la yeye kuhamia Manchester United na hawezi mtu akawa safarini kuelekea kaskazini na wakati huo huo akawa anacheza mpira "
"Hilo jambo ni gumu kabisa ndomana nikaamua kutompanga"
"Natarajia uhamisho wake utakamilika labda lakini siwezi kutangaza kwa sababu katika kipindi cha masaa 48 kutatolewa uwamuzi kwa njia moja au nyingine."
Alipoulizwa kuhusu mpango Wa kubadirishana na Henrikh Mkhitaryan, meneja huyo Wa Arsenal aliongeza: "mara nyingi hutokeaga tu kwa mchezaji kutoka timu moja kwenda nyingine na sio kubadirishana wachezaji na ndomana hii ya kubadirishana wachezaji inachukuwa muda mrefu kwasababu inahitaji kufuata utaratibu."
Bosi Wa Manchester United Jose Mourinho Ana matumaini na mpango huo kufanikiwa
"Natarajia unaweza kukamilika hivi karibuni au usikamilike kamwe" alisema baada ya United kushinda 1-0 dhidi ya Burnley."Nadhani mpango upo karibu, upo karibu saana kukamilika au inaweza tokea usikamilike kabisa lakini nna mtazamo chanya "
"Najua kwamba watu wangu wanafanya kila kitu ,kiukweli wanafanya kila linalowezekana,wamiliki wamewasha taa ya kijani, [mtendaji makamu mwenyekiti] Mr [Ed] Woodward anajitahidi kwa bidii saana."
"Nafikiri kila mtu anafanya kika linalowezekana na nadhani watafanikiwa."
"Tayari nimezungumza na mchezaji ? Hapana."
[Sky sport]