Emmanuel Adebayor "anaichukia" Arsenal kwa sababu ya "muongo" Arsene Wenger na anasema sikuzote "atampenda" Jose Mourinho
Kwa Sasa anachezea Uturuki, Adebayor anamlaumu Wenger juu ya jinsi yeye alivyokuwa akichukuliwa Kama mchezaji lakini anamsifu Bosi wake wa zamani wa Real MadridEmmanuel Adebayor ameiweka wazi "chuki yake" dhidi ya Arsenal ambayo inatokana na kujitoa kwake Arsenal kwasababu ya "muongo" Arsene Wenger.
mshambuliaji huyo mkubwa Wa zamani Wa Arsenal Adebayor alidai Wenger alikosa uaminifu ambapo unamfanya ampende Jose Mourinho, ambaye mshambuliaji huyo alicheza chini take wakati akiwa Real Madrid.
Na aliwaangazia mameneja wote ambao alicheza chini yao na hoja tata kuhusu kutoka kwake Arsenal na kwenda Manchester City katika mwaka 2009, Adebayor, kwa sasa anacheza kwa ajili ya Turkish leage leaders Istanbul Basaksehir, alisema: "Mourinho ni mmoja wa mameneja ambae nilimpenda na ntampenda daima
"Yeye ni mmoja wa mameneja waaminifu Sana ambao mimi nimekutana nao katika kazi yangu, ambapo Ni ajabu saana kwasababu mameneja wengi Sana sio wakweli (waongo) .
"Kama mfano, mimi nililikuwa na mkutano na Arsene Wenger katika ofisi yake aliniambia natakiwa niondoke alikuwa kwa sababu yeye haoni tena uwepo wangu Arsenal katika siku za mbeleni. Natakiwa niendelee na maisha yangu
"Mimi nilikuwa kama 'mimi nitaendelea kubaki.' Yeye Alikuwa kama 'hakuna hakuna hata hali yoyote ya kukubakiza hapa . Na hatuta fanya lolote ili uendelee kubaki . Wewe chagua kwenda timu nyingine au wewe kubaki hapa bila ya kupangwa katika mechi yeyote.'
"Hivyo mimi si kuwa njia nyingine yoyote ya kuchagua zaidi ya kujiunga na Man City ambayo nilifurahi sana kujiunga.
"Na siku ya pili wakati mimi nimejiunga na Manchester City nilimuona akifanya mkutano na waandishi wa habari London akisema kwamba nilitaka kuondoka kwa sababu fedha nilizopata zilikuwa nyingi na kila kitu na tangu siku hiyo ndipo nikawa na chuki dhidi ya Arsenal.
[Mirror]