jifunze kilimo cha matikiti

Habari ndugu, natumaini unaendelea vyema na juhudi za kuelekea kwenye mafanikio. Nina uhakika kabisa unatamani kutoka hapo ulipo na kufikia mafanikio, hata kama tayari umeshafikia kiwango fulani cha mafanikio  pia unatamani kusonga mbele zaidi.Leo ninataka tuanze kujifunza kuhusu kilimo maarufu kwa sasa hapa nchini ambacho ni kilimo cha tikiti maji. 


Kilimo cha tikiti maji katika jarida la fursa za kilimo, kilimo cha tikiti maji hakikosi katika majarida mbali mbali yanayo husu kilimo na hata katika kazi ninayofanya ya kutoa ushauri kwa wakulima, wakulima wengi wamekua wakitamani sana kujifunza na kuingia kwenye kilimo cha tikiti maji . 


Umaarufu na Kupendwa kwa kilimo hichi kunasababishwa na mambo mawili makubwa: 

(i) Ni kilimo cha muda mfupi (miezi 2 hadi 3) kiasi kwamba mkulima anaweza kulima hadi mara nne kwa Mwaka,

(ii) Mbegu na mahitaji yake ni rahisi kupatikana. 


pamoja na kwamba kuna changamoto zake, lakini ukiweza kufuata kanuni na kulilenga soko vizuri (timing ya soko) unaweza kupata kicheko cha pesa kizuri sana. 

Wapo wanaotengeneza faida zaidi ya milioni 5 kwa ekari na wapo wanaopata hasara pia. Sasa blog yako ya Kilimo biashara (www.kilimobiashara.net) inaanza kutoa mafunzo ya kilimo cha tikiti, tunaamini ukifanyia kazi mafunzo haya kupata faida kubwa kwenye zao hili itakua ni jambo la kawaida sana kwako. 

Fuatana nasi katika makala hizi za kilimo cha tikiti, hatukuelekezi tu jinsi ya kufanya, bali tunakufundisha pia ni kwanini kifanyike hivyo. Karibu sana!