Uvivu
uvivu hutokana na nini?
Mtu unaposhindwa kufikirisha ubongo na kutenda maamuzi  dhabiti,  hiyo ni dalili ya uvivu. Tatizo hili linakuwa  kubwa kwa sababu mbalimbali tokana na teknologia, mtu huyu yupo radhi akae aangalie Tv, Movies, aende club lakini asifanye jambo lolote la msingi la kujenga maisha yake, kwa kuona kwamba anapoteza mda. Watu wanasahu hili tatizo linazima ndoto kwa sababu yakupoteza muda kwa mambo yasiyo na maana  kwa wakat huo.

Marafiki,
Kuwa na marafiki ni jambo zuri katika maisha ya mwanadamu, kwa sababu tunahitaji watu kutupa mawazo mapya yatakayo kujenga kimaisha yako. Lakini je, jiulize una marafiki wangapi? ni wangapi kati ya hao ukiongelea maisha unaweza ona watakupa mawazo endelevu? je ni kweli wanaweza kusaidia wewe kufikia ndoto yako. cha kufanya  ni kuchagua marafiki walio bora watakaopigania maendeleo yako na kukuweka katika hali ya kujitoa  katika mambo yanayodidimiza ndoto yako.

Mapenzi
Mapenzi ni uwanja mpana sana ambao vijana wengi tunapitia na kuendelea nayo. Mapenzi yanaweza kuwa matamu na pia machungu kwa sabubu yanaumiza. Wapo wanaokata tamaa na maisha yao hadi kufikia hatua ya kujitoa duniani kwa sababu ya kuumizwa ama kusalitiwa na wapenzi wao, wengi hujiona hawana thamani katika hii dunia na hii inaweza kudhoofisha utendaji  wa kazi ofisini, hata nyumbani. Na hali inaweza kuwa mbaya zaidi pale uchumi unapoanza kudidimia, lakini unachopaswa kufahamu mapenzi yapo na ni jambo la kukaa na kufikiria maisha yako, kumuomba mungu akupe Mpenzi aje kuwa mke mwema au mme mwema mbeleni na kuendelea kupigania ndoto zako na malengo uliyojiwekea maishani.


                                                    Itaendelea......................................

0 Comments: