LIVE A PURPOSE TODAY

the most crucial element as human being is practicing helping other how to solve their problem we understand from our perspective that only thing that can be archived with grate execellency is helping other human to archive outmost best of their being.
we understand that as human race we have limited to pro exist in flesh adn body their for we must do our best to archive the most spectaticular of our being.

the only way you can trully be above all is through being the lowest among all
serve with excellence serve with humblenes , serve with a purpose of making other fill the love of unity and onenenes we m ust be our own love as for exterial power is love, all human requre is care nothing less nothing more only the fundamenaal nad practical sense of human being.

if the truly puprpose of being human being is helping others to reach their pottentials
rager that world without care it building without inhabitants
@aristidi valerian

USIKATE TAMAA TUTAFIKA.

Image result for youth african
Je ushAkaA ukafikiria jinsi binadamu tunavyounganishwa pamoja katika namna tofauti na  sana.
Kila kitu kinachokutokea kwenye maisha tambua huwa kina maana kubwa, tunaomba mungu tu mambo mabaya yasitujie, mungu huwa na njia nyingi sana za kutufanya Tu mkumbuke yeye katika nafasi zetu za maisha.
Kijana na kazi.
HEBU LEO TUJIULIZE NAMNA VIJANA WANAO NA TULIOMALIZA CHUO TUNAVYOPATA CHANGAMOTO KATIKA KUYAANZA MAISHA YA KUJITEGEMEA NA KUWA EGEMEO KWA WENGINE WALIO CHINI YETU.
MAMBO YAFUTAYAO NI BADHI YA MAMBO NILIYO JIFUNZA BAADA YA KUMALIZA CHUO KUNIWEZESHA KUANZA KUWA MwANFUNZI WA MAISHA NA MAENDELEO BINAFSI.
ü  JICHANGANYE NA WATU WOTE USIBAGUE.
ü  PENDA KUONGELEA TATIZO LAKO NA WATU WENGINE UTAONA MAFANIKIO.
ü  JIFUNZE KUANZA KUWEKA MAWAZO YA KUTUNZA FEDHA.
ü  USIKATE TAMAA.
ü  SAIDIA WENGINE KATIKA NAFASI YAKO.
ü  TUMIA KIPAJI CHAKO.
ü  FUATA NDOTO YAKO YA MDA MREFU.
ü  JITAHIDI KUPATA WATU WALIOKUZIDI ELIMU MAARIFA ZAIDI YAKO.
n.b ni vizuri kufahamu kuwa katika kila jambo kuna maendeleo hata katika hatua ndogo, sijafika nakualika nawe uwe shujaa katika safari hii.
 Image result for youth african


KIJANA WA SASA NA KAZI


BILA SHAKA KAZI NI MUHIMILI MKUBWA WA MAENDELEO KWA WATU WOTE KATIKA NCHI.
ila kwa asilimia kubwa changamoto ya kupata kazi katika sekta rasmi nayo imezidi kuongezeka hasa kwa kuwa na ufinyu wanfasi hizo kwa miaka ya karibuni
swali la kujiuliza lenye msingi mkubwa
je kijana awezaje kujipatia kipato katika sekta zisizo rasmi (ujasiriamali, kilimo, makampuni binafsi, utalii n.k)

majibu ya swali hili laweza kuwa mengi, ila amini kijana unayetafuta kazi ama kuanza shughuli binafsi wewe mwenyewe ndiye nguzo ya kujiinua

jichanganye na watu, eleza shida yako kwa watu ili upate upenyo na zaidi ya yote jitahidi kwa kadiri uwezavyo kutokata tamaa, ongeza bidii katika kutafuta kazi, funga na kuomba, ila zaidi kuwa mbunifu katika kufanya kazi binafsi hasa ujasiria mali, jitolee kwa makampuni nawe itakuwa rahisi kupata kazi.





KANUNI ZA FEDHA

KANUNI UNAZOTAKIWA KUZINGATIA KUHUSU FEDHA.
*KANUNI NO. 1*
Kamwe usikope fedha na hasa ya riba kwa ajili ya kuanzishia biashara (isipokuwa kwa mkopo ambao marejesho yake yanatokana na mshahara. Hii ni kwa sababu biashara huchukuwa muda mrefu kusimama yenyewe na kuanza kupata faida wakati marejesho ya mikopo mingi huanza mwezi baadaye ama hata kabla. Hivyo kamwe usikope mkopo ili
kuanzishia biashara ukitegemea hiyo hiyo biashara iweze kukulipia mkopo pamoja na riba yake.
*KANUNI NO 2*
Kamwe usitumie fedha ambayo bado  hujaipata / hujaimiliki. Wala usimuahidi mtu fedha kwa kutegemea fedha uliyoahidiwa na mtu mwingine. Usije ukamsikia mtu akikuambia "fulani njoo kesho ofisini kwangu saa 3 asubuhi uchukuwe shs. Milioni 2 halafu wewe akaenda dukani  kukopa vitu ukitegemea kulipa  utakapokuwa umechukua ile fedha uliyoahidiwa.
*KANUNI NO. 3*
Kama una nia ya kuweka akiba, kila upatapo fedha hakikisha huanzi kununua mahitaji yako kwanza kabla hujatenga fedha unayotaka kuweka akiba ukitegemea kwamba utaweka akiba kile kitakachobaki. Kwa kawaida huwa hakuna fedha inayobaki kwa sababu ilimradi fedha ya kutumia ipo, matumizi huwa hayakosekani na vitu ya kununua huwa vinaalikana lakini kama fedha ya kutumia haipo unaweza kutafuta njia nyingine ya kukabili changamoto zako. Ndiyo maana ni vema utaweka fedha ya akiba mbali kabisa na wewe na hiyo itakufanya ujione huna fedha kabisa.
*KANUNI NO 4*
Iwapo utapata fursa ya kukutana na watu mwenye mafanikio kiuchumi kamwe usiwaombe fedha. Waombe ushauri /waeleze  mawazo yako jinsi  unavyofikiri  namna utakavyofanya ili kupata fedha. Wanaweza wakaamua wao  mwenyewe hata kukupa fedha watakapoona kuwa mawazo yako ni mazuri na ya msingi. Lakini kamwe lengo lako lisiwe kupata fedha toka kwao.
*KANUNI NO 5*
Kamwe usitunze mbegu yako bila kuipanda. Watu wengi wanaishia kwenye kuweka akiba tu. Ni vigumu sana, kwa mfano kwa mfanyakazi, kuweka akiba tu na kupata mahitaji yote yatakayomfanya awe na kiwango kile kile cha maisha hasa hasa baada ya kustaafu. Unapoweka akiba hiyo ni mbegu; ipande. Unapoziweka tu mbegu nyingine huanza  kuoza (thamani yake huweza kupungua kwa sababu ya mfumuko wa bei na vitu kama hivyo.) Ndiyo maana ni vizuri kujifunza aina mbalimbali za uwekezaji unazoweza kutumia kukuza akiba yako. Hapa simaanishi kwamba lazima uwekeze kwenye biashara, kwa sababu unaweza kupoteza kirahisi fedha zako za akiba, hapa nazungumzia kuifanyia uwekezaji kama kununua hisa.
*KANUNI NO 6*
Kamwe usimkopee fedha mtu ambaye hutaki kumpoteza ama kukosana naye. Pale ambapo utamkopea hakikisha ndani ya moyo wako uwe umeamua kwamba ikitokea huyo mtu hajakulipa, hutakufa ukimnung'unikia huyo mtu. Wala hutampoteza huyo mtu kama rafiki. Kama utaona mtu utakaye mkopea anaweza akashindwa kurejesha mkopo na mkabaki marafiki basi mkopee. Lakini ukiona itakufanya hata  umchukie pamoja na hata ukoo wake tafadhali mshauri huyo rafiki aende  benki.
*KANUNI NO 7*
Kamwe usije akaweka sahihi yako kumdhamini mtu kwenye mambo ya fedha kama hutaki na hauko tayari kuja kumlipia huyo mtu hapo baadaye. Je unahitaji nieleze zaidi ya hapo kwa hili? Hapana, linajieleza lenyewe.
*KANUNI NO 8*
Epuka kuweka fedha ambayo hujapanga kuitumia  ndani ya kipindi kifupi sehemu ambayo inafikika kirahisi. Kwa mfano, usitembee na shs. Laki moja wakati ambapo ulichopanga kununua ama kufanya kinagharimu shs. Elfu ishirini tu. Utavikuta na kuvitamani  vitu ambavyo hukupanga kuvinunua ama kuvifanya.
* KANUNI NO 9*
Kamwe usitumie fedha kwa  kitu ambacho hakina ulazima kwako kwa wakati huo. Kabla hujatoa fedha yako kulipia kitu fulani hakikisha kwanza unajiuliza swali hili "kitatokea kitu gani kama sitanunua kitu  hiki?" Kama utaona unaweza kuishi vizuri na bila kuathirika na kukosekana  kwa kitu hicho tabasamu tu na ondoka zako,
* KANUNI NO 10*
Kamwe usifanye kitu ili kujionesha kuwa wewe ni tajiri. Kwa mfano kutumia shs elfu sabini kununua kitu kwa kuwa tu kinauzwa supermarket wakati kitu hicho hicho ungekipata Kariakoo kwa elfu thelathini. Kufanya hivyo ni kosa kubwa kikanuni isipokuwa kwa wale waliovuka kiwango cha hadhi ya kifedha kimaisha.
* KANUNI NO 11
Kamwe usiwe na tabia ya kutumia kipato chako chote ama zaidi ya kipato chako. Kufanya hivyo ni sawa na kuwa na tanki la maji lenye bomba dogo la kuingizia maji wakati hilo tanki lina  bomba kubwa la kutolea. Hata siku moja haliwezi kujaa. Na ikawa bomba la kuingizia maji litaendelea kupungua ukubwa wake ndivyo ambavyo tanki litaisha maji haraka. Lakini ukifanya kinyume chake yaani bomba kubwa liwe la kuingizia maji na lile dogo liwe la kutolea, hapo maji yatajaa na kufurika. Hivyo  hakikisha kila wakati na muda wote unaongeza ukubwa wa bomba linaloingiza na kupunguza bomba linalotoa.
*KANUNI NO 12*
Kamwe usiwe na mipango ya muda mfupi tu na kusahau kuwa na mipango ya muda mrefu pia na wala usikazanie kuwa mipango ya muda mrefu tu ukasahau kuwa pia na mipango ya muda mfupi. Dada mmoja aliambiwa ardhi ni mali. Basi akakusanya fedha kwa muda mrefu akanunua heka 30 za ardhi. Kwa sasa ana ardhi  lakini hana hela za matumizi wala za kuendeleza ardhi yake na haoni  hata jinsi ambavyo atatumia ardhi yake ili apate fedha hata kwa siku za usoni. Hebu jiulize; kuwa na heka 30 za ardhi huku huna fedha ya chakula kwa familia yako au ya kumpelekea mtoto wako hospitali huo ni utajiri au umaskini? Nadhani huyu dada alijali zaidi mipango ya muda mrefu akasahau mipango  ya muda mfupi. MUNGU TUBARIKI HAYA YAWE MEMA

WANYAMA KUMI HATARI ZAIDI DUNIANI



BAADHI YA WANYAMA TUNAOWAJUA KUWA NI WAZURI KWA MWONEKANO AU UMBO, NI BAADHI YA WANYAMA HATARI ZAIDI DUNIANI KWA  KUSABABISHA VIFO KWA WANADAMU KWA NAMNA ZIFUATAZO.

1.DOLPHIN- HUZAMISHA  NDANI YA  MAJI BILA YA KUWA NA SABABU MAALUMU(WAKIAMUA TU)

2.MBWA- KUNGATA WATU

3. SOKWE MTU- HOUONGOZA KWA KUSHAMBULIA WATU USONI NA MIKONI HADI KUWAUA

4. DUBU-- HUWEZA KUVUNJA VUNJA MIFUPA YA WANADAMU KWA KUNGATA NA MENO YAO

5. TEMBO- HUONGOZA KWA  KUWAUA  BINADAMU KWA KUWA VUNJA VUNJA

6. PWEZA- WENYE RANGI RANGI HUWA NA SUMU KALI MABAYO HUSABABISHA KIFO KWA BINADMAU

7. VYURA--- WANASUMU KALI HASWA VYURA WENYE RANGI ZA BLUE PAMOJA NA GOLD HUWEZA KUUWA WATU 20 NA KWA DAKIKA CHACHE TU.

Soko la Ajira

Soko la ajira limekumbwa na changamoto nyingi sana Tanzania, haswa kwa wananchi waliokuwa wanatarajia kuajiriwa katika sekta rasmi za serikali pamoja na sekta binafsi kutokana na ubadilikaji wa sera ya nchi,

Mabadiliko katika nyanja zote ni muhimu ili jamii iweze kuishi vyema, bila mabadiliko yenye mauvumivu kidogo kwa ajili ya kupata mafanikio yasiyoisha kwa nchi nzima kwa siku za mbeleni hatuwezi kufika mbali,  KUTOKA KWA MWANDISHI CHARLES DARWIN  1864 ,mabadiliko hutokea na ni lazima yatokee, ila watu wawezao kupita salama katika mfumo wa mabadiliko sio wenye fedha san, sio wenye akili sana, sio wenye vyeo sana, ila wale wenye uwezo wa kundeana na mabadiliko.

 Je mi na wewe tunaweza kupitaje katika kipindi hiki cha mabadiliko hilo ni swali kubwa tunalopaswa kujiuliza, bila shaka fikra za kuweza kuendana na mfumo ni niyngi je twaweza, kufanikiwa

 jibu langu ni ndiyo,  pale tu tutakapoendana na mabiliko na kuangalia fursa zinazopewa kipaumbele na madhumuni ya mabadiliko.
  Image result for positive change for development

FURSA UZALISHAJI WA MIWA

Kutokana na ongezeko la watu na ukuaji wa kipato miongoni mwa watanzania, ukuaji wa soko la sukari Tanzania unakadiriwa kufikia asilimia 6% kwa mwaka. Upungufu wa usambazaji wa sukari kwa sasa unakadiriwa kufika tani 300,000.
Takwimu hizi zinategemewa kupanda kwa kasi kwa sababu wazalishaji wa sukari waliopo hawajaongeza uwezo wao wa kuzalisha kulingana na ukuaji wa mahitaji. Mbali na upungufu huo ndani ya Tanzania, upungufu wa sukari kwa soko la Afrika Mashariki unakadiriwa kufikia tani 400,000 kwa mwaka. Kwa kuzingatia hayo uzalishaji wa sukari ni fursa ambayo wajasiriamali kwa ujumla wanatakiwa kuitumia ili kujiongezea kipato. Mikoa kama Kagera na Morogoro ndio mikoa ambayo kilimo cha miwa kinashamiri vizuri.

ufugaji wa kuku wa kienyeji



Ufugaji wa kuku wa kienyeji(kuku Asili): kanuni bora za ufugaji

        1 comment:
Dondoo za ufugaji bora wa kuku wa asili

Ufugaji wa kuku wa asili ni nyenzo muhimu katika kupambana na wimbi la umasikini kwa kuongeza kipato cha kaya. Hata hivyo, pamoja na soko la uhakika, bado ufugaji kuku haujaweza kutumika ipasavyo kupambana na umaskini unaowakabili Watanzania wengi. Ni mazoea kwa jamii nyingi hapa Tanzania kufuga kuku wa asili kama sehemu ya mila na desturi zao. Kuku wa asili amekuwa akifugwa bila ya kupatiwa huduma muhimu kama makaazi bora, chakula cha ziada, tiba, kinga za magonjwa mbali mbali. Muhtasari huu unatoa muongozo wa ufugaji wa kuku wa asili ili uweze kuzalisha na hatimae kukuza kuku kwa wingi.
 http://ufugajimakini.blogspot.com/
Dondoo ya 1
Usafi wa vyombo na mazingira ya kuku
Uchafu ni mama wa magonjwa, hivyo zingatia haya;
1.  Vyombo vya chakula na maji visafishwe mara kwa mara kwa maji safi na sabuni.
2.  Pumba au chakula kilicholowana na kuchanganyika na kinyesi cha kuku kitolowe na kufukiwa.
3.  Choma moto au zika kwenye shimo refu kuku waliokufa kwa ugonjwa.
4.  Usifuge kuku na ndege wa jamii nyingine kwa mfano bata katika banda moja.
5.  Ondoa mbolea mara kwa mara kutoka katika banda la kuku.
6.  Tumia dawa za kuulia vimelea kusafishia banda na upake chokaa angalau mara moja kwa mwaka.
7.  Ziba matundu yote yanayoweza kuruhusu panya na wanyama wakali kama vicheche kuingia katika banda la kuku.
Dondoo ya 2
Magonjwa na kinga kwa kuku wote
Ndui ya kuku
Huathiri sana vifaranga wanaokua na ujitokeza kwa wingi wakati wa mvua za muda mrefu. Husababisha vivimbe katika uso/ kishungi na hata sehemu nyengine zisizo na manyoya.
Mdondo/kideri
Mdondo, au kwa majina mengine lufuo, au kideri ni ugonjwa hatari katika magonjwa ya kuku wa asili. Ni ugojwa wa virusi ambao huathiri kuku wa rika zote, huweza kuangamiza kuku wote kijijni.
Ukosefu wa vitamini A
Ugonjwa huu husababisha macho kuvimba na kutoa uchafu mziito kama sabuni iliyolowana. Kuku wenye dalili hizi hawaponi na hata kufa. Ugonjwa hujitokeza baada ya kipindi kirefu cha kiangazi kwa ajili ya ukosefu wa majani mabichi.
Kosidiosisi
Huathiri kuku wa umri wowote lakini huuwa zaidi vifaranga na kuku wanaokua. Kuku hudhoofika, manyoya huvurugika na kuku huwa kama wamevaa koti. Kuku huarisha damu au kinyesi cha kahawia na huzubaa na kuonekana kama wamevaa koti.
Viroboto, chawa na utitiri
Hawa ni wadudu wa nje wanaoshambulia ngozi. Huweza kusababisha ugonjwa kutokana na kunyonya damu. Viroboto hushambulia kichwa na kunata huku wakinyonya damu. Viroboto huuwa vifaranga. Chawa na utitiri hughasi kuku hadi wakashindwa kutaga na kuatamia.
Minyoo
Minyoo huweza kudhofisha kuku na kuwafanya waweze kuugua maradhi mengine kirahisi. Muone mtaalaam ukihisi kuku wako wana minyoo.
Dondoo ya 3
Chakula cha ziada
1.  Wapatie vifaranga nyongeza ya protini kwa kuwachanganyia vumbi la dagaa au vichwa vya dagaa vilivyotwangwa kwenye pumba za mahindi.
2.  Changanya kikombe kimoja cha vumbi la dagaa na vikombe vitano vya pumba za mahindi (tumia kikombe kidogo cha chai).
3.  Mchwa na wadudu wengine wanaweza kutumika kama nyongeza ya protini.
4.  Vuna mchwa kwenye vichuguu au tengeneza mchwa katika njia za mchwa.
5.  Kutengeneza mchwa: changanya kinyesi cha ng’ombe na majani makavu, mabua ya mahindi au maranda ya mbao katika chungu au ndoo ya zamani.
6.  Mwagia maji hadi kila kilichomo kilowane kisha weka katika chombo kama ndoo au chungu. Weka chombo chako katika njia ya mchwa ukikigeuza juu chini na subiri hadi kesho yake asubuhi, kisha beba vyote vilivyomo na uwamwagie kuku mahali walipo.
Dondoo ya 4
Utotoleshaji wa vifaranga
Chagua jogoo bora na tetea bora kuzalisha kuku.
Sifa za jogoo bora
1.  Awe na umbo kubwa, awe ukiko mzuri na usioangukia upande mmoja.
2.  Apende kuwa na himaya yake. Ukimpata jogoo mwenye sifa hizi mueke yeye na matetea kumi. Hivyo ukiwa na matetea ishirini jogoo wawili wanatosha.

Sifa za tetea bora
Tetea bora ni yule mwenye umbo kubwa, mwenye uwezo wa kutaga mayai ya kutosha, kuatamia na hatimaye kutotoa vifaranga.
Uhifadhi wa mayai
1.  Weka mayai mahali safi na penye hewa ya kutosha.
2.  Tumia kasha lililokatwa na kujaza mchanga mkavu na safi au kasha la kuhifadhia mayai.
3.  Weka sehemu butu ya yai iwe upande wa juu na ile iliyochongoka itizame chini.
4.  Andika namba au tarehe katika siku lilipotagwa.
5.  Mayai yakishatagwa yatolewe na kuhifadhiwa na moja liachwe kwenye kiota ili kumuita kuku kuja kutaga kesho yake.
Kuatamiza mayai
1.  Kuku awekewe mayai yatakayokuwa na uwezo wa kuyaatamia na kuyatotoa yote.
2.  Mayi 10 hadi 12 yanatosha kuatamia.
3.  Mayai ya kuatamiza yasizidi wilki 2 toka kutagwa.
4.  Yai la mwisho kutagwa liwe la kwanza kuchaguliwa hadi yapatikane mayai 10 mpaka 12, na apewe kuku wa kuyaatamia.
5.  Mayai ya kuatamiza yasafishwe kwa kitambaa kikavu na safi au kilichowekwa spiriti
Kutotolesha vifaranga wengi kwa wakati mmoja
1.  Kama unataka kuku zaidi ya mmoja watamie na kutotoa kwa mpigo fanya yafuatayo;
2.  Kuku wa kwanza akianza kuatamia muwekee mayai yasiyo na mbegu mfano mayai ya kuku wa kisasa au kuku asiye na jogoo.
3.  Rudia zoezi hilo hadi utakapofikisha kuku watano kisha wawekee kuku wote mayai yenye mbegu.
Dondoo ya 5
Matunzo ya vifaranga ili kuzuia vifo
Vifaranga wengi hufa kabla ya kufikisha miezi miwili kutokana na magonjwa, baridi na kuliwa na wanyama wengine. Ili kupunguza vifo vya vifaranga wa siku 1 hadi miezi miwili zingatia yafuatayo;

Ulinzi dhidi ya mwewe na wanyama wengine
1.  Weka vifarang kwenye tega na kuwafunika ili wasinde mbali wakati wa mchana. Wape maji na chakula. Hakikisha hawapigwi jua wala kunyeshewa mvua. Wakati wa usiku walale na mama yao.
Chanjo ya mdondo kideri/lufuo
Kama tetea alichanjwa kabla ya kuanza kutaga vifaranga wanaoanguliwa huwa na kinga ya mdondo ya kuwatosha kwa wiki 3 za kwanza za maisha yao. Wachanje vifaranga hao dhidi ya mdondo wafikishapo umri wa siku 18.
Vifaranga ambao historia ya chanjo ya mama haijulikani, wapewe chanjo ya mdondo siku tatu baada ya kuanguliwa, rudia hadi wakifikisha wiki tatu kisha uchanje kila baada ya miezi 3
Kinga dhidi ya kosidiosisi
Kinga ya kosidiosisi kwa vifaranga, itolewe hata kama ugonjwa haujajitokeza.
1.  Wape dawa ya amprolium kwa muda wa siku tatu mfululizo mara wafikishapo siku saba tokea waanguliwe kama kinga ya kosidiosisi.
2.  Dawa inaweza kutolewa hata kama wamevuka umri huo. Fuata maelekezo ya mtaalam juu ya kiasi cha dawa kinachopaswa kuchanganwa katika maji au pumba
3.  Kama vifaranga wadogo wataonesha dalili za kuzubaa kama kuvaa koti wapewe dawa ya amprolium kwenye maji kwa utaratibu ufuatao;
Dawa siku tatu mfululizo: usiwape kwa siku mbili; gawa tena kwa siku tatu

Hitimisho
1.  Hakikisha banda na vyombo vya chakula cha kuku ni visafi kuepusha magonjwa.
2.  Usichanganye kuku na bata katika banda moja
3.  Lisha chakula cha ziada hasa kwa vifaranga.
4.  Kideri, kosidiosisi, ndui na upungufu wa vitamini A ni vyanzo vikuu vya vifo vya kuku wako. Kumbuka kukinga kuku wako dhidi ya magojwa haya.
5.  Kumbuka kuchagua mayai ya kuatamiza kama ilivyoelekezwa ili kuepuka kupata mayai viza.
6.  Vifaranga wadogo hadi wiki nane huhitaji matunzo mazuri, fuata maelezo kuzuia vifo.
7.  Kumbuka ukiuza kuku wengi kwa mpigo utaongeza mapato yako, jitahidi kuzalisha vifaranga kwa wingi ili upate kuku wengi baadae.
8.  Muone mtaalam wa mifugo ulie karibu nae kwa ushauri zaidi.
9.  Soma maelezo haya mara kwa mara na ufanye yalioelekezwa.
10.              Washirikishe wengine katika kaya yako ili nao wajifunze na kufanya hivyo kukuza ufugaji na kipato cha familia.




CREDITS TO KAVISHE VICTOR